Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, maonesho ya “Mega Education Fair” ya Taasisi ya Anfal yaliandaliwa kwa ushiriki mpana wa wanafunzi wa vyuo, wazazi, walimu na watu wa tamaduni katika ukumbi wa Qaisar Bagh Dongri mjini Mumbai.
Mwanzoni mwa maonesho hayo, banda maalumu lilitengwa kwa ajili ya kuwakumbuka mashahidi wanafunzi wa Shule ya Shajarat Tayyiba Minab. Katika banda hilo, jina na picha ya kila shahidi viliwekwa ndani ya begi dogo ambalo liligawiwa kwa wanafunzi.
Chanzo: Idara ya Uhusiano wa Umma ya Shirika la Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu.
Maoni yako